KUKATA UTEPE

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akikata utepe kuzindua rasmi maabara 10 zinazohamishika kwenye hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), Matthius Kamwa, Mwakilishi wa Bodi ya ushauri ya Mamlaka ya Dawa na Chakula nchini (TFDA), Zainab Thabit na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Hiiti Sillo

Add a comment

AKIJENGA OFISI

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) akijenga Ofisi ya walimu Shule ya Msingi Kichangani Kata ya Majohe Manispaa ya Ilala wakati wa Uzinduzi wa Ujenzi Ofisi 402 ulioanza jana.

Add a comment

PORI TENGEFU LOLIONDO

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akitembelea eneo la Pori Tengefu la Loliondo wilayani Ngorongoro mkoa wa Arusha juzi, kujionea mambo mbalimbali kuhusu mgogoro wa muda mrefu katika eneo hilo. (Picha na Michuzi Blog).

Add a comment