KUTUMIA APP

Mwanafunzi wa darasa la kwanza Shule ya Kimataifa, Dar es Salaam, DIS, Ethan Yona akiwaelekeza watoto wenzake namna ya kutumia App (zana) yake ya EthanMan inayomwezesha mtumiaji kusoma kitabu chake kwa njia hiyo ya mtandao, tukio hilo lilifanyika juzi kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika viwanja vya Michezo vya Jakaya Kikwete, Kidongo Chekundu Dar Es Salaam. (Na Mpigapicha Wetu).

Add a comment

KUSOMA QUR-AN

Mmoja wa watakaoshiriki mashindano ya Dunia ya kusoma na kuhifadhi Qur-an, Omar Abdallah Salim wa Tanzania (kulia) akisoma Qur-an kwa waandishi. Mashindano hayo ya 25 yanayoshirikisha nchi 19 yanatarajiwa kufanyika leo jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni, Laeeq Hattas (Afrika Kusini), Tahmil Murtafi (19) Bangladesh. (Picha na Yusuf Badi).

Add a comment

MAANDAMANO

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mbeya wakiandamana ndani ya Uwanja wa Ofisi za Chama hicho huku wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe tofauti wa kumpongeza Rais John Magufuli kwa maamuzi magumu na yenye tija kwa taifa anayoyachukua ikiwemo kuwawajibisha watu walioshiriki katika wizi wa dhahabu nchini. (Picha na Joachim Nyambo).

Add a comment

KUWASILISHA MADA

Meneja wa Huduma za Utalii wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Philip Chitaunga (kushoto) akiwasilisha mada kuhusu shughuli za taasisi hiyo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) katika semina iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, mjini Dodoma jana. (Picha na Hamza Temba - WMU).

Add a comment

MKUTANO

Wakuu wa wilaya, wakurugenzi watendaji na maofisa kilimo wa wilaya 33 za mikoa tisa inayolima pamba wakiwa katika mkutano wa wadau wa zao hilo jijini Mwanza jana. (Na Mpigapicha Wetu).

Add a comment