MKESHA WA KRISMAS KURASINI

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo amewataka wakristo wote na watanzania kwa ujumla kudumisha amani kwa sababu ni tunu inayoliliwa na mataifa yote ulimwenguni. Alikuwa akitoa salamu za Krismasi katika Mkesha uliofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Maurus Kurasini jijini Dar es Salaam.

Add a comment

KIVUTIO KINGINE KIPYA KILICHOPO KONDOA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Dk James Wakibara (mbele) akiongoza timu ya maofisa wengine wa mamlaka hiyo, iliyotafiti na kugundua mwamba mkubwa ulio kwenye Hifadhi ya Swaga Swaga wilayani Kondoa ukiwa na michoro ya zamani ya Warangi na Wasandawe na kufanya kuwa kivutio kingine kipya kilichopo Kaskazini. (Picha na Marc Nkwame).

Add a comment

MAZOEZI YA UKAKAMAVU

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro (kushoto mbele) akifanya mazoezi ya ukakamavu na askari wa kikosi cha kupambana na uhalifu mkoa wa Lindi baada ya kumaliza ukaguzi wa kikosi hicho akiwa kwenye ziara yake ya kikazi mkoani humo jana.

Add a comment

AKIPANDA MTI

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akipanda mti baada ya kuzindua kampeni ya kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa kijani iliyofanyika kwenye chanzo cha maji cha Bonde la Makutupora mjini humo jana.

Add a comment