ZAWADI

Waziri wa Elimu, sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako akimpa zawadi mwanafunzi aliyefanya vyema kitaifa kutoka shule ya Sekondary ya St Mary Mazinde Juu, iliyopo Lushoto, Editha Msenga wakati wa maadhimisho ya siku ya elimu yaliyofanyika katika shule ya sekondari ya wasichana ya Msalato, Dodoma jana. Mwingine (kushoto) ni mwakilishi wa wabia wa maendeleo Caroline.

Add a comment

KUPOKEA TAARIFA

Rais John Magufuli akipokea taarifa ya Kamati ya pili ya wachumi na wanasheria ya uchunguzi wa madini yaliyopo kwenye makontena yenye mchanga wa madini (Makinikia) kutoka kwa Mwenyekiti wake, Profesa Nehemia Osoro, Ikulu, Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.

Add a comment

AKISIKILIZA TAARIFA

Rais John Magufuli alipokuwa akisikiliza taarifa ya Kamati ya pili ya wachumi na wanasheria ya uchunguzi wa madini yaliyopo kwenye makontena yenye mchanga (Makinikia) kabla ya kukabidhiwa Ikulu, Dar es Salaam.

Add a comment

KUTOA MADA

Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), inayochapisha magazeti ya Daily News, HabariLeo na SpotiLeo, Dk Jim Yonaz akitoa mada wakati wa Kongamano la Pili la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi linalofanyika Mjini Dodoma na kuandaliwa na Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC). Kauli mbiu ya Kongamano hilo ni Wezesha Watanzania Kushiriki Uchumi wa Viwanda.

Add a comment