SALAMU

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe akisalimiana na viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kagera katika ziara yake mkoani humo kuzungumzia operesheni ya kuondoa mifugo kwenye maeneo ya hifadhi pamoja na taratibu sahihi za kuendesha minada ya mifugo iliyotaifishwa kisheria juzi mjini Bukoba. Anayeongoza utambulisho huo ni Mkuu wa mkoa huo, Salum Kijuu. (Picha na Wizara ya Maliasili).

Add a comment

UHARIBIFU - BARABARA

Wakati mvua za masika zikielekea ukingoni katika maeneo mengi nchini, kwa jiji la Dar es Salaam zimefanya uharibifu wa miundombinu katika manispaa ya Ilala hususani jimbo la Ukonga ambapo barabara zake nyingi zimeharibika kama hii ya Mkolemba hadi Kapungu. (Picha na Mroki Mroki).

Add a comment

MKATABA WA USHIRIKIANO

Wakiwa katika tukio la kusaini mkataba wa ushirikiano kati ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji wa Kiuchumi (NEEC) na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) katika kuandaa kongamano la pili la uwezeshaji wananchi kiuchumi litakalofanyika mjini Dodoma, mwaka huu. Aliye kulia ni Mhariri Mtendaji wa TSN, Dk Jim Yonazi.

Add a comment

KIAPO.

Viongozi mbalimbali wakila kiapo cha uadilifu baada ya kuapishwa na Rais John Magufuli, Ikulu, Dar es Salaam jana. Kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Tixon Nzunda, Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Rajab Luhwavi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa, Benard Makali, Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Geoffrey Mwambe. (Picha na Ikulu).

Add a comment