KUPANDA MTI

Wanafunzi wa shule binafsi ya msingi ya Little Treasure wakishiriki kwa pamoja kupanda mti wa kumbukumbu ya ziara yao katika Kituo cha Kulelea Watoto Walemavu wa Ngozi kilichopo Buhangija Manispaa ya Shinyanga. Katika ziara hiyo pia waliwapelekea madaftari. (Picha na Kareny Masasy).

Add a comment

ZIARA MITAMBO YA KUFUA UMEME

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia uzalishaji, Mhandisi Abdallah Ikwasa (kushoto) akimpatia maelezo Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani alipotembelea mitambo ya kufua umeme ya Kinyerezi 1 jijini Dar es Salaam jana kufuatia kukatika umeme katika maeneo mbalimbali nchini yaliyounganishwa kwenye gridi ya Taifa. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu (Nishati), Dk. Juliana Palangyo. (Na Mpigapicha Wetu).

Add a comment

KIKAO - MPANGO KAZI

Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein (kushoto) akizungumza na uongozi wa Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo katika kikao cha siku moja cha utekelezaji wa mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika katika ukumbi wa Ikulu, mjini Unguja jana. (Picha na Ikulu).

Add a comment

MAFUNZO YA KUJIOKOA BAHARINI

Wanafunzi wa Chuo cha Bahari nchini (DMI) wakielea majini huku wameshikilia boya kubwa la kujiokolea lenye uwezo wa kushikwa na watu 12 wakati wakitoa mafunzo ya kujiokoa inapotokea ajali majini kwa abiria wanaotumia kivuko cha Magogoni Kigamboni Dar es Salaam. Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na kufanyika jana. (Na Mpigapicha Wetu).

Add a comment