HATI ZA MKATABA

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), Profesa Sylvester Mpanduji (kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Dk Bwire Ndazi wakibadilishana hati za mkataba wa makubaliano wa kutoa mafunzo na mikopo kwa wajasiriamali kwa lengo la kuwaandaa na kuwajengea uwezo kuelekea katika uchumi wa viwanda katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam juzi. Wa pili kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dk Adelhem Meru na maofisa mbalimbali wa mamlaka na shirika hilo.

Add a comment

KUZUNGUMZA

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, (IGP) Ernest Mangu akizungumza na waandishi wa habari akiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi la Angola, Paulo de Almeida (kushoto) na Mkuu wa Jeshi la Polisi la Msumbiji, Paulo Chachine (kulia) wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kutoka nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO) uliofanyika jijini Arusha jana. (Picha na Hassan Mndeme, Jeshi la Polisi).

Add a comment

UHARIBIFU - BARABARA

Mvua zinazoendelea kunyesha sehemu mbalimbali nchini zimesababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara na kufanya magari ya abiria na mizigo kukwama mara kwa mara njiani kama yalivyokutwa magari haya Mavimba, Tarafa ya Lupiro, wilayani Ulanga mkoani Morogoro hivi karibun. (Na Mpigapicha Wetu).

Add a comment