KUPOKEA MIILI YA ASKARI WALIOUAWA DRC

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk Hussein Ali Mwinyi (kulia) akiongoza askari wa jeshi hilo wakati wa kupokea miili ya askari 14 waliouawa nchini DRC wiki iliyopita. Miili ya askari hao ilipokelewa kwenye Uwanja wa Jeshi (Air Wing) Dar es Salaam jana. (Picha na Iddy Mwema).

Add a comment

KUSAINI NYARAKA ZA MSAMAHA

RAIS John Magufuli akitia saini nyaraka za msamaha alioutoa kwa wafungwa 61 waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa
Magereza, Juma Malewa akishuhudia tukio hilo lililofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mjini Dodoma.

Add a comment

KUANGALIA KIATU

Rais John Magufuli akiangalia ubora wa kiatu cha Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Melkior Komba, Katika Ikulu ya Chamwino Dodoma. Viatu hivyo vimetengenezwa na kiwanda cha Jeshi la Magereza Karanga kilichopo Moshi mkoani Kilimanjaro. (Picha na Ikulu).

Add a comment

DAR ES SALAAM KIDEDEA

Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita (wa pili kulia) akiwa na viongozi wengine huko Chicago nchini Marekani wameshika tuzo zao baada ya Dar es Salaam kuwa miongoni mwa majiji 10 duniani ambayo yamepata tuzo ya C40 Bloomberg Philantropies 2017, kupitia Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (UDART). (Picha na Christina Mwagala).

Add a comment

KUTETA JAMBO

Spika wa Bunge, Job Ndugai (kulia) akiteta jambo na Spika wa Bunge la Morocco, Habib El Malk, nyumbani kwake mjini Dodoma baada ya kumalizika kwa maadhimisho ya miaka 56 ya uhuru wa Tanzania Bara. (Picha na Ofisi ya Bunge).

Add a comment

AKIONESHA BOMBA LA KAMPUNI YA TIPER

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye akionesha bomba la Kampuni ya Tiper ambalo linatumika kupitisha mafuta yasiyounganishwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari ya Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Deusdedit Kakoko.

Add a comment