KUWEKWA WAKFU

Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam, Jackson Sosthenes Jackson akiwekwa wakfu na kusimikwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana nchini Dk Jacob Chimeledya katika Kanisa Kuu la Anglikana Mt. Albano, Upanga Jijini jana. (Picha na Ikulu).

Add a comment

KUKAGUA GWARIDE

Amiri Jeshi Mkuu, Rais John Magufuli akikagua gwaride la maofisa wapya wa Jeshi la Ulinzi pamoja na baadhi kutoka nchi marafiki kabla ya kuwatunuku Kamisheni katika viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam jana. (Picha na Ikulu).

Add a comment

KUTUNUKU KAMISHENI

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli akiwatunuku Kamisheni Maafisa wapya 192 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania pamoja na Maafisa kadhaa kutoka nchi marafiki katika Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.

Add a comment

KUVALISHANA VYEO

Mafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi wakivalishana vyeo mara baada ya Kutunukiwa Kamisheni na Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli katika viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Add a comment

UZINDUZI AWAMU YA TATU USAMBAZAJI UMEME

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa Nne kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Br. Gen. Mstaafu Emanuel Maganga (wa Tano kushoto), Mbunge wa Muhangwe ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Atashasta Nditiye (wa pili kushoto), Mbunge wa Buyungu, Kasuku Bilago (wa Kwanza kushoto) wakifunua kitambaa kuashiria uzinduzi wa Mradi wa usambazaji umeme vijijini Awamu ya Tatu katika wilaya za Kibondo na Kakonko.

Add a comment