Shule Kilwa zakabiliwa na uchakavu

SHULE za msingi pamoja na sekondari wilayani Kilwa mkoani Lindi zinadaiwa kuwa chakavu yakiwemo majengo, madarasa, vyoo na ofisi za walimu.

Hali ambayo imesababisha kuahatarishi kwa wanafunzi na walimu kudondokewa na kuta wakati wakiwa mashuleni mwao. Diwani wa Kata ya Singino, Said Arobaini aliyasema hayo jana wakati wa kikao cha kuwasilisha taarifa za kata katika baraza la madiwani.

Alisema kuna shule ya msingi ya Kivinje iko upande wa baharini na ina hali mbaya, hivyo inahitaji uboreshaji kwa majengo yake ni machakavu na yamechoka. Hata hivyo, alisema mamlaka iliweza kutumia Sh milioni 6 kufanyia ukarabati baadhi ya shule hizo.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Fransis Kaunda alikiri kuwapo uchakavu huo. Alisema kwamba kuna umhimu kuwapo mpango shirikishi wa kuweza kutatua kero hizo za mashule.

Kaunda ambaye ni Ofisa Mipango wa mamlaka hiyo alisema kwamba wananchi, halmashauri zishirikiane, hayiwezeka ili kuweza kumaliza kero hizo. Alisema kwamba kuwepo mpango maalumu wa kujenga majengo au ukarabati wananchi walichangia kiasi fulani na mamlaka nayo inamalizia pale ilipoishia jamii husika.