Daraja la Mto Momba latengewa milioni 3/-

SERIKALI imetenga Sh milioni tatu kwa ajili ya ujenzi wa daraja la Mto Momba linalounganisha kata ya Kamsamba katika jimbo la Momba na kata ya Kipeta katika jimbo la Kwela mkoani Songwe.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani alitoa maelezo hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Momba, Davidi Silinde (Chadema), lililoulizwa kwa niaba yake na Mbunge wa Tunduma, Frank Mwakayoka (Chadema). Mbunge Silinde aliuliza lini ahadi ya serikali ya kujenga daraja hilo iliyotolewa mwaka 2009 itakamilishwa.

Ngonyani alisema mwaka wa fedha 2016/17, serikali ilitenga Sh bilioni 2.9 katika bajeti yake na kwamba hivi sasa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) wapo katika hatua za mwisho za kumpata mkandarasi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa daraja hilo.

Alisema serikali kwa kufahamu umuhimu wa daraja hilo, itaanza ujenzi wa daraja la Momba ambalo ni kiungo muhimu katika barabara hiyo katika mwaka huu wa fedha. Ngonyani alisema daraja la Mombo ni kiungo muhimu katika barabara ya Kibaoni-Kasansa-Muze-Ilemba- Kilyamatundu-Kamsamba hadi Mlowo ambayo inaunganisha mikoa mitatu ya Katavi, Rukwa na Songwe.

Alisema barabara hiyo ni kiungo muhimu kati ya mikoa hiyo kwani inapita katika bonde la Ziwa Rukwa ambalo ni maarufu kwa uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo