Wakata mikoko kukiona

MKUU wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa amesema atahakikisha anapambana na wenyeviti wa mitaa wanaowafi cha wanaojihusisha na ukataji mikoko kwa ajili ya shughuli za uchomaji mkaa.

Akizungumza jana aliwataka wenyeviti hao wafanye kazi kwa kushirikiana na ofisi yake pamoja na Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), wilaya za Temeke na Kigamboni kwa kutoa taarifa ili wahalifu wakamatwe mara moja. Aidha, Mgandilwa amewaagiza TFS wafanye doria za mara kwa mara.