Kortini kwa kukutwa na sare za JWTZ

MKAZI wa Tabata, Casto Gongo (35) amefi kishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na makosa matatu ikiwemo la uhujumu uchumi pamoja na kukutwa na sare za Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Gongo alifikishwa mahakamani hapo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba Wakili wa Serikali, Simon Wankyo alidai Juni 15, mwaka huu mshitakiwa huyo alikutwa na sare za JWTZ katika eneo la Gako Inland Container Depot (ICD) iliyopo Sokota Chang’ombe.

Inadaiwa Juni 15, mwaka huu, mshitakiwa alikutwa na Ofisa wa Polisi akiwa na bidhaa kinyume cha sheria katika Bandari Kavu.