Wezi wa mtandao wawatesa mapadri

PADRI Paschal Luhengo wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mahenge, Parokia ya Lupiro wilayani Ulanga mkoani Morogoro ameiomba serikali kuingilia kati na kutokomeza wimbi la wezi wa mtandao ambalo limeibukia kuwaumiza baadhi ya watawa, mapadri na watu wengine.

Alitoa ombi hilo hivi karibuni mara baada ya Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mahenge , Agapit Ndorobo kumaliza ibada maalumu ya kubariki jengo la Zahanati ya Kanisa la Parokia ya Lupiro iliyojengwa kwa ufadhili na Chama cha Sauti cha Uingereza (Hampshire Scouts , Uk ) kupitia Tawi la Mamba.

Luhengo ni mmoja wa waathirika wa kuibiwa na wezi wa mtandao na alisema kuwa wezi hao wamekuwa wakiingilia mawasiliano ya barua pepe za watawa na mapadri zinazozitumika kuwasiliana na marafiki na wafadhili wao nje ya nchi wakiomba fedha na kuingiziwa kupitia benki hapa nchini.

Kwa mujibu wa Padri huyo, vitendo vya kuibiwa kwa njia ya mtandao vilifanyika kati ya Septemba mwaka 2016 hadi Aprili mwaka huu ambapo mara ya kwanza aliibiwa dola za Marekani 20,000 na mara ya pili dola za Marekani 8,000. Mmoja wa watuhumiwa amefungua kaunti kwa jina la Parokia yake kwenye moja ya benki hizo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro , Ulrich Matei alisema katika taarifa yake ya mkoa hakuna tukio hilo la mapadri kuibiwa na alipowasiliana kwa simu na Askofu Ndorobo wa Jimbo la Mahenga, alimfahamisha matukio hayo ya yametokea Jijini Dar es Salaam