Serikali, ATCL washauriwa kupuuza 'wachumia tumbo'

KAMATI ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakili Zanzibar limeishauri serikali na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kuacha kubishana na wachumia tumbo badala yake kuweka mikakati ya kuhakikisha shirika hilo linafanya vizuri.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Suleiman Sahran Said amegtoa kauli hiyo leo wakati kamati hiyo ilipotembelea makamo makuu ya shirika hilo jijini Dar es Salaam. "Bora kwenda taratibu lakini tufike kwa wakati kuliko kukimbia ili kuwafurahisha watu. Wanasiasa waiopenda maendeleo wapo kila sehemu, sisi tusonge mbele," amesema Said.