Watumishi wa SMZ wajengewa uwezo APRM

WATENDAJI wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), wanajengewa uwezo waweze kuoanisha Mpango Kazi wa Mpango wa Kujitathmini kwenye eneo la Utawala Bora Barani Afrika (APRM) na mipango ya Maendeleo ya Zanzibar.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ilisema watendaji hao watajengewa uwezo kupitia warsha itakayoendeshwa Agosti 24 na 25 na watoa mada kutoka Zanzibar na kwenye mataifa mengine ikiwemo Ghana, Afrika Kusini, pamoja na kutoka katika Shirika la Mandeleo la umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mpango wa Kupunguza Umasikini na Kuleta Maendeleo Namba III ni miongoni mwa mipango ambayo watendaji hao wanawezeshwa waweze kuioanisha.

Warsha hiyo inaelezwa pia kuwa itajadili namna ya kuunganisha mipango ya maendeelo ya nchi, ajenda 2063 ya Umoja wa afrika, malengo endelevu ya milenia pamoja na Mpango Kazi wa APRM, uzoefu wa nchi nyingine za kiafrika katika kuunganisha mipango yao ya maendeleo na Mpango Kazi wa APRM na Mkakati wa Tathmini na Ufuatiliaji.