Rais Magufuli avunja Mamlaka ya Usimamizi wa Mji Mdogo wa Kigamboni

RAIS John Magufuli amevunja Mamlaka ya Usimamizi wa Mji Mdogo wa Kigamboni (KDA) ambapo kuanzia sasa shughuli zote zilizokua zikifanywa na mamlaka hiyo zitafanywa Manispaa ya Kigamboni.

Hatua hiyo imekuja kutokana na mkanganyiko wa kimajukumu uliokuwepo kati ya KDA na Manispaa ya Kigamboni. Uamuzi huo ulitangazwa leo na Waziri Lukuvi alipotembelea Kigamboni na kuzunhumza na wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wa Manispaa hiyo