Kitilya aendelea kusota rumande

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya baada ya upande wa mashitaka kuomba kuongezewa siku 14 kwa ajili ya kueleza upelelezi wa kesi hiyo ulipofikia.

Wakili Mwandamizi wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi amedai, awali waliomba siku 14 kwa ajili ya kueleza mwenendo wa kesi hiyo lakini wameshindwa kufanya kazi hiyo katika muda walioomba hivuo wapewe siku 14 nyingine.

Hata hivyo, Wakili wa washitakiwa hao, Dk Masumbuko Lamwai amedai ni zaidi ya mwaka mmoja tangu kesi hiyo ilipofunguliwa lakini bado upelelezi haujakamilika. Amedai kuwa kesi ya utakatishaji fedha iliwekwa kwa nakusudi ili wateja wake wakae gerezani na kwamba licha ya mahakama hiyo kuwa haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo lakini upande wa mashitaka unatumia vibaya taratibu za kimahakama.

Hakimu Mfawidhi Cyprian Mkeha amewaambia washitakiwa kuwa, upelelezi unaendelea kufanywa na kwamba amejidhihirisha unakaribia mwisho hivyo waendelee kuwa na imani. Wengine katika kesi hiyo ni mshindi wa Miss Tanzania mwaka 1996, Shise Sinare na Sioi Solomon...mnaomba chekin hayo majina vizur hata kwenye google