Serikali kupiga mnada ng’ombe 10,000

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dk. Luhaga Mpina ametanga kupiga mnada ng’ombe zaidi ya 10,000 wa kutoka nchi za Rwanda na Uganda ambao wamekamatwa katika operesheni ya siku saba inayoendelea nchin.

Mpna aliyasema hayo wakati akijivu hoja zilzoibuliwa na wabunge ambapo amesema ng’ombe hao watapgwa mnada kama ilivyokuwa kwa ng’ombe 1,325 wa kutoka nchin Kenya ambao walikamtwa baada ya kungia nchini.

Akichangia Mpango wa Maendeleo ya Tafa wa mwaka 2017/2018, Waziri Mpina amesema, wapo watu wanaosema kuwa hatua hiyo inaweza kuvuruga mahusiano ya nchi za Afrika Masharki ambapo amesisitiza kuwa uhusiano wan chi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uko imara na hauwez kuvurugwa na uhalifu.

“Hakuna ushirika wa uhalifu, watu wanaoingza mifugo kutoka nje ya nchi ni wahalifu kwasababu wamevunja sheria…mhalifu akija hapa hawezi kutetewa kwasababu ya ushirika, ushirika wetu sio wa uhalifu, mashirikiano yetu ni mazuri kwasababu yapo ksheria,” amesema.