Shehe Dar ataka maadili kujenga imani

SHEHE wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum amewataka wasomi nchini kuelimisha jamii kuhusu maadili ili kujenga jamii yenye imani.

Aliyasema hayo katika mahafali ya wanachuo na wanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Seminari ya Al- Haramain, jijini Dar es Salaam. Shehe Salum aliwataka wahitimu hao kuwa na maadili yanayoendana na elimu yao ili jamii inayowazunguka iweze kuiga kutoka kwao.

Aliongeza kuwa wasomi wanatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha jamii inajifunza katika misingi bora na yenye weledi katika maisha yao ya kila siku. Mkuu wa Chuo cha Al-Haramain, Mwalimu Suleimani Urassa aliliomba Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) kuwasaidia kukabili upungufu wa madarasa.