‘Ujangili umekuwa mwiba kwa wanyamapori wadogo’

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi amesema ujangili wa wanyamapori wadogo pamoja na mimea bado ni tatizo.

Alisema ni tatizo kwa kuwa mbinu nyingi za kupambana na ujangili zinazotumika kwa sasa zimejikita katika kupambana na majangili wa wanyamapori wakubwa kama vile tembo na faru, lakini wale wanyamapori wadogo hawajalindwa ipasavyo.

Milanzi alisema hayo Dar es Salaam jana wakati akifungua mkutano wa kimataifa wa kujadili mbinu za kupambana na ujangili uliokutanisha wahifadhi wa wanyamapori kutoka nchi za Zambia, Kenya, Malawi na Botswana, lengo likiwa ni kukuza ushirikiano katika mapambano dhidi ya ujangili katika maeneo ya mipakani.

Milanzi amewataka wataalamu wa uhifadhi wa wanyamapori waanze kuona namna gani wataweza kugundua mbinu za kuanza kupambana na majangili wanaoua wanyamapori kwa ajili ya nyama ya kula (kitoweo).

Alisema kumekuwa na juhudi mbalimbali zinazochukuliwa na mataifa mbalimbali duniani katika kupambana na ujangili wa wanyamapori wakubwa kama vile tembo, faru na nyati, lakini wanyama wadogo kama mijusi, ndege pamoja na mimea midogo imekuwa ikipotea lakini hakuna yoyote anayejali