'OPRAS imeimarisha utendaji kazini'

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya jiji la Tanga, Daudi Mayeji amesema ufanisi kazini wa watumishi wa idara mbalimbali umeongezeka baada ya kuanza kutumia kwa karibu mfumo wa kutathmini utendajikazi wa wazi (OPRAS) unaoweka bayana majukumu na malengo ikilinganishwa na ilivyokuwa awali.

Ametoa kauli hiyo wakati akiwasilisha taarifa ya utendaji wa halmashauri hiyo kuhusu Utumishi na Utawala Bora kwa Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika alipotembelea baadhi ya wanufaika wa utekelezaji wa miradi ya TASAF III jijini Tanga.

Mafanikio hayo amesema yametokana na hatua ya wilaya kuwekwa wazi majukumu ya kazi, malengo ya utendaji, watumishi wote kukubali kuongozwa na maadili ya ufanyaji kazi wa pamoja, uwajibikaji kwa ngazi zote pamoja na Utawala Bora. MWISHO