Ombi la wafanyabiashara wa Tangamano kusikilizwa

MKUU wa wilaya ya Tanga, Thobias Milapwa amewaahidi wafanyabiashara wa gulio la Tangamano kwamba amepokea na atafikisha kwenye mamlaka husika ombi lao linaloitaka halmashauri ya jiji kupunguza ushuru kutoka sh. 1,500 mpaka 500, kurasimisha na kuboresha mazingira ya eneo hilo ili wawezekuchangia ipasavyo maendeleo ya nchi.

Alikuwa akizungumza na wafanyabiashara hao ili kuzindua mradi wa kuendesha semina za kutoa elimu kwa mlipakodi mkoani Tanga inayolenga kuwatambua na kuwasajili wafanyabiashara walio katika sekta isiyo rasmi inayoratibiwa na mamlaka ya mapato (TRA).

"Ninachoweza kusema kuhusu ombi lenu hilo nimelipokea lakini uamuzi wake sinao hapa kwasababu niwa kisera hivyo lazima lipitie mchakato wa maamuzi ya watu wanaotajwa kisheria vikiwemo vikao vya baraza la madiwani wa Halmashauri ya jiji la Tanga", alisema.