Profesa Kabudi akamilisha kanuni sheria ya madini

Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amewasilisha vitabu vya kanuni za sheria ya madni namba 7 ya mwaka 2017 kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi baada ya kukamilisha kanuni hizo.

Profesa Kabudi akiwa na Naibu Mawaziri wa Madini, Stanslaus Nyongo na Doto Biteko amesema, kanuni hizo zimekamilika siku moja kabla ya tarehe ya mwisho iliyotolewa na Rais John Magufuli na kubainisha kuwa kwa sasa sheria inaweza kuanza kutumika.

Kwa upande wao Naibu Mawaziri wa Nishati wamewataka Watanzania na wadau wote wa sekta ya madini kushirikiana na Serikali kutekeleza sheria hiyo na wamempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kutoa msukumo wa kukamilishwa kwa kanuni hizo.