Viongozi watakaodharau mahakama 'kukiona'

JAJI Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahimu Juma amesema watakuwa wakali na kuwachukulia hatua viongozi watakaoingilia Mahakama kwani ndio iliyopewa mamlaka ya kutoa haki.

Jaji Profesa Juma ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Wiki ya Sheria itakayoanza Januari 27, 2018 hadi Januari 30, 2018.

Amesema kuwa viongozi wengi hawaheshimu amri zinazotolewa na mahakama hivyo kusababisha muingiliano wa mihimili na kuwashauri kila mtu abaki katika maeneo yao waliyopewa mamlaka ya kikatiba.

Kaulimbiu ya wiki hiyo ni matumizi ya Tehama katika utoaji haki kwa wakati na kuzingatia maadili Rais Mstaafu Jakaya Kikwete atafungua maadhimisho hayo Januari 27, mwaka huu katika viwanja vya Mnazi Mmoja.