Wanafunzi 465 washindwa kuripoti kidato cha kwanza

WANAFUNZI 465 hawajaripoti katika shule walizopangiwa kuanza kidato cha kwanza mwaka huu wilayani Mbarali mkoani Mbeya kutokana na sababu zisizojulikana.

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Mfune alibainisha hayo kwenye kikao cha baraza maalumu la kupitisha mapendekezo ya bajeti ya mwaka wa fedha ujao.

Mfune aliagiza hatua za kisheria kwa wazazi wote ambao watoto wao hawajaripoti katika shule walizopangiwa ili kuwawezesha kuanza masomo.

Alisema wanafunzi waliochaguliwa walikuwa 3,025 kati yao, wavulana ni 1,524 na wasichana ni 1,501 na hadi sasa, walioripoti ni 2,308 wakati waliobadili shule ni wanafunzi 100 na wengine 152 wamekwenda katika shule binafsi