Ajali yaua watano Tanga, sita wajeruhiwa

Watu watano wamefariki papo hapo, wengine sita wamejeruhiwa baada ya basi la kampuni ya AJ Safari lililokuwa linatokea Lushoto kwenda jijini Dar es Salaam kugongana uso kwa uso na basi dogo aina ya Hiace katika kijiji cha Kabuku, wilayani Handeni.

Polisi mkoani Tanga imethibitoisha kutokea kwa ajali hiyo takribani saa sita mchana leo na miongoni mwa waliofariki dunia ni dereva wa Hiace hiyo wakati wenzake wa basi kubwa amepata majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake. Majeruhi walikimbizwa katika Kituo cha Afya cha Kabuku kwa ajili ya matibabu wakati miili ya waliofariki katika ajali hiyo imepekwa Hospitali ya Magunga wilayani Korogwe.