Watakiwa kuweka benki ya matofali

MWENYEKITI wa Halmashauri ya wilaya ya Uyui mkoani Tabora, Said Ntahondi amewataka watendaji wa kata na vijiji kuweka benki ya matofali kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kiserikali, vinginevyo hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.

Agizo hilo limetolewa katika kikao cha baraza la madiwani kilichoketi juzi. Mwenyekiti huyo alimtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Uyui, Hadija Makuwani kuwaandikia barua watendaji wa kata na vijiji kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hilo la baraza ambalo linatakiwa kutekelezwa haraka.

Ntahondi alisema, benki hiyo ya matofali itasaidia katika shughuli mbalimbali za kijamii na kiserikali hasa ujenzi kwa maendeleo ya kata hizo.