Wanawake wainuliwe kiuchumi - Viongozi

VIONGOZI mbalimbali akiwemo Mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli wametoa mwito kwa mashirika ya umma, sekta binafsi, asasi za kiraia na watu binafsi, kushirikiana na serikali katika kuwawezesha wanawake kwa kuwapatia mbinu mbalimbali za mafunzo, mitaji na kuwatafutia masoko ya bidhaa zao.

Walisema hayo kwenye Maadhimisho ya Siku ya Waanawake Duniani jana. Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mama Janeth alisema serikali imejitahidi kuweka usawa wa jinsia na kuwezesha wanawake kisiasa, kiuchumi, elimu na afya, lakini serikali pekee haiwezi kumaliza changamoto zote, hivyo ni lazima wananchi wenyewe washiriki. Aidha alisema kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ambayo ni ‘Kuelekea Uchumi wa Viwanda Tuimarishe Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji wa Wanawake Vijijini’, imeendana na nia ya dhati ya serikali ya awamu ya tano ya kujenga Tanzania ya viwanda.

Aliupongeza mkoa huo kwa kuwa na vikundi 400 vya wanawake, ambavyo vinajishughulisha na shughuli mbalimbali, ikiwemo usindikaji, ushonaji, utengenezaji sabuni na shughuli nyingine. Alitoa mwito kwa mikoa mingine nchini, kuiga mfano huo ili kuwezesha wanawake kiuchumi ikiwemo kwenye shughuli za ujenzi wa viwanda.

“Ni imani yangu kuwa kama mikoa yote pamoja na taasisi nyingine za serikali zitaiga mfano huu, basi tutaweza kuwezesha wanawake kiuchumi pamoja na ujenzi wa viwanda,” aliongeza. Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda alisema kwamba mkoa huo unaendelea kuboresha sekta ya afya kwa ajili ya kuwasaidia akina mama, ikiwemo ujenzi wa hospitali za mama na mtoto. Alisema lengo ni kuhakikisha hakuna mwanamke, anayepoteza maisha wakati wa kujifungua.

“ Tayari tumejenga hospitali ya mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Amana Wilaya ya Ilala, Chanika na wodi ya kujifungulia iliyopo Hospitali ya Mwananyamala. Tumepata Sh bilioni 18 kwa ajili ya kujenga hospitali ya mama na mtoto katika wilaya za Ubungo na Kigamboni,” alisema. Aidha, alisema ili kuwafuta machozi wanawake ambao watoto wao wamejiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya, vita na kampeni ya mapambano dhidi ya dawa za kulevya imewezesha vijana 6,000 kuachana na dawa hizo.

WATAKIWA KUWEKA JITIHADA BINAFSI

Katika hatua nyingine, wanawake nchini wametakiwa kutumia jitihada binafsi katika kujikwamua kimaisha, hasa kwa kujitathmini na kuyafanya yale yaliyo ndani ya uwezo wao. Mwito huo ulitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mradi wa Maadili ya Uongozi, Scholastica Kimario, alipokuwa akitoa mada kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo kwa Wanawake wenye Mafanikio nchini (TWAA) katika maadhimisho hayo jana. Mratibu wa Tuzo za TWAA, Irene Kiwia aliitaka serikali kutekeleza sera za kumuendeleza mwanamke ili Tanzania iwe yenye mafanikio katika uimarishwaji wa nyanja zote za usawa wa kijinsia.

WATAKIWA WASIOGOPE

Mwanasiasa mkongwe nchini, Zakhia Meghji aliwataka wanawake kutoogopa kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi nchini, kwa kuwa kwa asili wao ni viongozi. Alisema, “Kwa kuwa wanawake ni viongozi wa asili yaani pale nyumbani anaweza kujua mipango yote ya ndani inavyotakiwa kwenda na kuisimamia, sasa hata ikiwa katika uongozi wa kisiasa tunaweza kinachotakiwa ni kutoogopa na kukata tamaa”.

UKATILI KUISHA INAWEZEKANA

Huko Rombo mkoani Kilimanjaro, imeelezwa kuwa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili kwa Wanawake na Watoto (MTAKUWA), utafanikiwa iwapo kutakuwa na ushirikiano mzuri miongoni mwa washiriki wa mpango huo. Shirika lisilo la kiserikali linaloshughulika na masuala Na Sophia Mwambe MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka wanawake wote ambao wametelekezwa na waume zao na kubeba majukumu ya kulea watoto peke yao, wafi ke ofi sini kwake Aprili 9, mwaka huu kwa ajili ya kupatiwa msaada wa kisheria. Alisema hayo jana wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, ambayo kimkoa yalifanyika wilaya ya Ubungo.

Alisema kumekuwa na ongezeko kubwa la wanawake, ambao wanalea watoto peke yao wakati wenza wao wapo, lakini hawatoi msaada wowote. ‘’Unakuta mwanamume anamsababishia mwanamke afukuzwe nyumbani kwa sababu ya kupata mimba, wengine wanafukuzwa na ndugu zao, wengine wanahangaika kulea watoto peke yao na mwanaume yupo.

Hivyo nataka mfike ili muweze kupatiwa msaada wa kisheria,’’ alisema Makonda. Alisema tayari ameshapitia sheria ya malezi na kuona matakwa ya sheria hiyo kwamba watoto wanapaswa kulelewa na wazazi wote wawili kwa kushirikiana; na sio kumuachia mzigo mama peke yake. ‘’Moyo wangu umebeba huzuni ya akina mama ambao wanateseka nataka mpate haki yenu ya malezi ninachowaomba wanawake endeleeni kuliombea Taifa, Rais na viongozi wengine wa serikali ili waendelee kuwasaidia kupata usawa wa kijinsia,’’ alisema Makonda. ya sheria na haki binadamu mkoani Kilimanjaro (Kwieco), lilisema kuwa ukatili wa kijinsia unaweza kuisha ifikapo 2022.

Mwezeshaji kutoka Kwieco, Hillary Tesha alisema,”Lengo litakuwa ni kutokomeza ukatili kwa wanawake na watoto kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2022, kila aliyeshiriki mpango huu atatakiwa kuonesha mchango wake alioutoa katika kuutekeleza mpango huu.”

CHANGAMOTO ZA KINAMAMA ZITATULIWE MAPEMA

SERIKALI ya mkoa wa Morogoro imekusudia kutoa kipaumbele kwa akinamama na vijana katika kutatua changamoto wakulima ili kupata maeneo ya kilimo, waweze kuongeza tija katika mazao ya chakula na biashara. Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Stephen Kebwe alisema jana wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, iliyoandaliwa na Muungano wa Vikundi vya Wakulima Wadogo Tanzania (MVIWATA) katika viwanja vya ofisi ya Kijiji cha Rudewa Gongoni wilayani Kilosa. Alisema, “Tutawapa kipaumbele wanawake, na pia watapata haki kwenye masuala ya ardhi kwani wana haki ya kuhudumiwa na kupewa nafasi kama ilivyo kwa watu wengine.”

MIFUMO KUWEKWA KWA NYADHIFA

Pamoja na jitidihada zinazofanywa na wadau mbalimbali katika kumkomboa mwanamke, wameonekea kuwa mfumo wa nyadhifa ukiwekwa utasaidia wanawake. Akizungumza na kinamama wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Morogoro katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wanawake, jana, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Lughano Kusiluka alisema kuwa suala la ukombozi kwa wanawake, linahitaji kuwekewa taratibu za kimfumo. Kusiluka alisema kuwa chuo hicho kwa kwa kumthamini mwanamke, wameweka mpango mkakati ambao ulianza kutekelezwa tangu mwaka jana ikiwemo uendelezaji usawa wa kijinsia ambapo alisema kuwa yeye kama mkuu wa chuo amefanya uteuzi katika nafasi za juu kwa kuwapa wanawake na kwamba hawajamuangusha.

WANAWAKE WAZEMBE WAADHIBIWE

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameshauri wanawake wazembe kuchukuliwa hatua iwe kama adhabu. Akiadhimisha siku hiyo maalumu ya wanawake akiwa mjini Sumbawanga mkoa wa Rukwa, Waziri Ummy alimshauri Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchia aielekeze Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), iwafikishe mahakamani watumishi wote wa Benki ya Wanawake Tanzania ili ukweli ujulikane kuhusu kufa kwa benki hiyo.

Alisema watumishi wa benki hiyo , wanatuhumiwa kuisababishia benki hiyo hasara kubwa kutokana na matumizi mabovu ya ofisi na ufisadi. “Wanawake wenzetu tuliowaamini kuongoza Benki ya Wanawake nchini wametuangusha, wameshindwa kabisa kuiendesha benki hii kutokana na utendaji wao mbovu na ufisadi… “… Tayari tumeshafikisha majina yao Takukuru hivyo namuomba sana Waziri George Mkuchika aielekeze Takukuru iwafikishe mahakamani ili ukweli,” alisisitiza.

SEKTA BINAFSI IANGALIE WANAWAKE

SERIKALI imezitaka kampuni za sekta binafsi kushirikiana na Soko la Hisa kuweka mazingira, yatakayoendeleza usawa wa kijinsia kwa kuchukua njia jumuishi ya kufungua nguvu za wanawake katika biashara na jamii. Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sihaba Nkinga alisema hayo katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

WANAWAKE WASAIDIANE

Akihutubia baada ya kupokea maandamano ya wanawake Mkoa wa Dodoma katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Mbunge wa Viti Maalumu, Fatma Tawfiq, alisema wanawake wenyewe wana jukumu kubwa la kuinua uchumi wao na kuwainua wanawake wengine. Tawfiq aliwataka wanawake kutambua na kutumia fursa za kiuchumi katika maeneo yao na kuinuana wao kwa wao, huku akimpongeza Rais Magufuli na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kwa kuhimiza uanzishwaji wa jukwaa za uwezeshaji wanawake ambazo zitakuwa mkombozi kwa wanawake.