Makisio ya bajeti ijayo ni trilioni 32.5

Serikali imepanga kukusanya na kutumia trilioni 32.475 kwa mwaka wa fedha ujao wa 2018/2019.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango ameweka hayo bayana leo wakati akiwasilisha makisio hayo kwa wabunge mjini Dodoma leo. Kwa mujibu wa Waziri Mpango, bajeti ya miradi ya maendeleo inatarajiwa kuongezeka kwa asilimia nane na kufika trilioni 12.007 kutoka trilioni 11.999 zilizopangwa kutumiwa katika mwaka huu wa fedha 2017/18.