Polisi: Mwanafunzi ‘aliyetekwa Dar’ alikuwa kwa mpenziwe Iringa

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa ameeleza kuwa uchunguzi wa awali umebainisha kuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Abdul Nondo alikwenda Iringa kwa mpenzi wake, hivyo hakutekwa.

Hivyo, Jeshi la Polisi Dar es Salaam kwa kushirikiana na lile la Iringa linamshikilia mwanafunzi huyo kwa madai ya kuzusha kuwa alitekwa. Linatarajiwa kumfikisha mahakamani kujibu tuhuma hizo.

"Uchunguzi ulibaini kuwa mwanafunzi huyo hakutekwa bali alijiteka mwenyewe ili kutafuta umaarufu wa kisiasa na kusababisha kuzua tafrani kwa jamii,” Mambosasa amesema leo jijini Dar es Salaam.

Kamanda amebainisha kuwa, upelelezi uliendelea na kubaini kua mwanafunzi huyo alikwenda kwa mtu aliyedaiwa kuwa mpenzi wake, ambaye alikuwa akifanya naye mawasiliano mara kwa mara akiwa njiani kuelekea Iringa.

Amesema kuwa Jeshi la Polisi limebaini hayo baada ya kupata taarifa za kutekwa kwa kijana huyo kupitia mitandao ya kijamii lilifanya uchunguzi ili kubaini ukweli wa taarifa hizo