Rais wa zamani atupwa kwa miaka 24

Aliyekuwa rais wa zamani wa Korea Kusini, Park Geun-hye amehukumiwa kwenda jela kwa muda wa miaka 24 baada ya kukutwa na hatia ya matumizi mabaya na ufisadi.

Pamoja na kifungo hicho, kwa mujibu wa BBC, mwanasiasa huyo amepigwa faini ya Won za Kikorea bilioni 18, sawa na dola za Kimarekani milioni 17, baada ya mahakama kumkuta na hatia ya ufisadi.

BBC imeendelea kuripoti kuwa, Park aligomea shauri la kesi yake, hata kufikia hatua ya kukituhumu chombo hicho kuwa maamuzi yake yanaegemea upande mmoja. Hata hivyo, alikanusha mashitaka dhidi yake na kusema hajafanya makosa yoyote. Hatua ya kurusha maamuzi ya kesi hiyo moja kwa moja kupitia vituo vya luninga imelaumiwa lakini wapo wanaodhani kuwa tukio hilo lilikuwa na maslahi mapana ya umma.