Luhaga Mpina ateketeza zana haramu za uvuvi za bilioni 2

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ametaifisha na kuteketeza zana haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni 2 zilizokamatwa wakati zikitumika kwa shughuli za uvuvi katika visiwa vidogo vilivyopo ndani ya Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza huku Shilingi milioni 120 zikikusanywa kama sehemu ya adhabu kwa wavuvi na wafanyabiashara waliokutwa na zana haramu pamoja na makosa ya utoroshaji samaki na mazao yake nje ya nchi.

Add a comment