Azam si riziki Caf

WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Azam jana waliaga michuano hiyo baada ya kuchapwa mabao 3-0 na Mbabane Swallows ya Swaziland.

Habari kutoka Mbabane zinasema mechi hiyo ilijaa vurugu, hali iliyosababisha wachezaji wa Azam kuvalia kwenye gari.

Azam ilijiweka pagumu kwenye michuano hiyo baada ya kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0.

Matokeo hayo sasa yanairudisha Azam nyumbani kujipanga upya kuwania nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao.

Akizungumzia mechi hiyo msemaji wa Azam, Jaffar Iddi alisema wamekubali matokeo na sasa wanarudi nyumbani kujipanga kwa michuano mingine inayowakabili.