Katibu BFT bado njia panda

KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Ndondi Tanzania (BFT), Makore Mashaga bado hajaamua hatma yake katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Desemba mwaka huu.

Akizungumza kwa simu na mwandishi wa habari hizi, Mashaga alisema juzi kuwa, bado hajaamua kugombea au kutogombea uongozi BFT.

Mashaga na viongozi wenzake walipo madarakani, waliingia uongozini miaka minne iliyopita katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Bagamoyo.

Hatahivyo, chini ya uongozi wake, BFT imeshindwa kupeleka timu katika mashindano ya ndondi ya Afrika na yale ya dunia sababu ya ukata.

Na tayari kiongozi huyo ameshatangaza kuwa mwaka huu hawana uhakika wa kupeleka timu katika mashindano ya Afrika Brazzaville, Congo nay ale ya dunia Humburg, Ujerumani.

Alisema sababu kubwa ni ukata kwani kila wanapopiga hodi kuomba msaada wamekuwa wakikosa.