Beno Kakolanya amrithi Dida Taifa Stars

KIKOSI cha wachezaji 23 cha Timu ya Taifa (Taifa Stars) kitakachoivaa Lesotho katika mechi ya kirafiki mwezi ujao kimetajwa leo jijini Dar es Salaam ambapo kwa mara ya kwanza kipa namba mbili wa Yanga amechukua nafasi ya Deogratius Munishi ‘Dida’.

Akizungumza na wandishi wa habari mda mfupi uliopita, Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga alisema wachezaji wataingia kambini na mazoezi yataanza Mei 24-29 Dar es Salaam na Mei 30 watakwenda kuweka kambi Misri kwa wiki moja.

“Baada ya mechi za mwisho za Ligi Kuu Tanzania Bara ambazo zitafika tamati wiki hii timu timu itaingia kambini Dar es Salaam kabla ya Mei 30 kwenda Misri kuweka kambi ya wiki moja itarudi Juni 7 kwa ajili ya mechi dhidi ya Lesotho,” alisema Mayanga.

Katika orodha ya majina ambayo Mayanga ametaja jina la Dida limeachwa na badala yake amechukuliwa kipa wa Yanga, Benno Kakolanya baada ya kufanya vizuri katika mechi za mwisho za Ligi Kuu na kuisaidia timu hiyo kutetea ubingwa.

Kikosi kamili cha Taifa Stars

Makipa ni Aishi Manula, Benno Kakolanya, Said Mohammed

Mabeki ni Shomari Kapombe, Hassan Kessy, Mwinyi Haji Mngwali, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Salim Abdallah, Aggrey Morris, Abdi Banda na Erasto Nyoni.

Viungo ni Himid Mao, Jonas Mkude, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Said Ndemla, Muzamil Yassin, Simon Msuva, Farid Mussa na Shiza Kichuya.

Washambuliaji ni Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta, Mbaraka Yussuf, Ibrahim Ajib na Abdulrahman Mussa.

Benchi la ufundi ni Kocha Mkuu Salum Mayanga akisaidiwa na Fulgence Novatus, kocha wa makipa, Patrick Mwangata, Meneja ni Dani Msangi, Madaktari Gilberti Kigadiya na Richard Yomba na mtunza vifaa Ally Ruvu.