Samatta awania tuzo za mchezaji bora Afrika

Mtanzania Mbwana Samatta anayechezea klabu ya Genk ya Ubelgiji ni miongoni mwa wachezahi 30 wanaowania tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) latangaza leo.

Kwa mujibu wa CAF, mshindi wa tuzo hiyo ataamuliwa na kura kutoka kwa makocha wakuu, wakurugenzi wa mabenchi ya ufundi, wajumbe wa kamati ya ufundi CAF na jopo la wataalam kutoka vyombo vya habari.

Tuzo hiyo inatarajiwa kutolewa Januari 4, mwaka ujao jijini Accra, Ghana, CAF imeongeza katika taarifa yake iliyotoka leo Jumatano. Katika kinyang’anyiro hicho, wachezaji wengine kutoka Afrika Mashariki waliotajwa kuwania tuzo hiyo ni Mganda Michael Olunga na Mganda Denis Onyango.

Aidha, CAF imetaja majina mengine 30 ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora kwa wachezaji wanaocheza ndani ya bara la Afrika.