Yanga hasira zote kwa Mwadui

KOCHA Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa amesema mawazo yao yote wameyahamishia katika mchezo wao ujao dhidi ya Mwadui na kwamba sio wa kuubeza, wanahitaji kujipanga kupata ushindi.

Yanga ilirejea Dar es Salaam Alhamisi, ikitokea Zanzibar baada ya kutolewa kwenye michuano ya Mapinduzi hatua ya nusu fainali dhidi ya URA kwa mikwaju wa penalti 5-4. Jumatano ijayo wanatarajiwa kucheza mchezo wa raundi ya 13 wa Ligi kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili, Nsajigwa alisema kikosi kitaanza mazoezi kesho kujiandaa na mchezo huo muhimu kwao katika mbio za kutetea taji la ligi. “Tunautazama mchezo huo ni muhimu kwetu kupata matokeo, kama unavyojua kwenye ligi hakuna timu ndogo, ni lazima tupambane kupata matokeo mazuri,” alisema.

Alisema Mwadui ni timu nzuri na ina wachezaji wazuri hivyo, iwapo wataibeza inaweza ikawaumbua. Yanga huenda ikalipiza kisasi kwa Mwadui kwa kuhakikisha wanapata matokeo mazuri baada ya mchezo uliopita wa ligi dhidi ya Mbao FC kuchapwa mabao 2-0 huko jijini Mwanza.

Kutokana na matokeo hayo yaliyopita Yanga ilibaki na pointi 21 ikishika nafasi ya nne kabla ya michezo ya jana, ikiwa nyuma ya Singida United yenye pointi 23. Iwapo itaruhusu kupoteza mchezo huo kuna uwezekano wa kuendelea kushuka