Man United kupambana na Brighton robo fainali

KLABU ya Manchester United itacheza dhidi ya Brighton katika mchezo wa robo fainali wa Kombe la FA. Timu hizo zilipambana katika fainali ya michuano hiyo mwaka 1983.

Mshindi wa mchezo utakaozikutanisha Tottenham huko Rochdale jana atakutana na Sheffield Jumatano au Swansea, ambaye atacheza baada ya suluhu ya jana Jumamosi.

Southampton leo itasafiri na kucheza na mshindi kati ya Manchester City na Wigan, wakati Leicester na Chelsea watakutana katika mchezo utakaozikutanisha timu za Ligi Kuu.

Rochdale, timu ya chini kabisa iliyobaki katika mashindano hayo, iko mkiani katika Ligi Daraja la Pili, jana ilitarajia kucheza dhidi ya Tottenham. Wigan, iliyopo katika nafasi ya pili katika Ligi Daraja la Pili, itacheza dhidi ya Manchester City leo Jumatatu.

Leicester, ambayo iliifunga Sheffield United 1-0 Ijumaa, itakuwa na kibarua kigumu wakati itakapocheza dhidi ya Chelsea, ambao nao walishinda Ijumaa kwa mabao 4-0 dhidi ya Hull City.

Ratiba ya robo fainali ya FA Cup Leicester v Chelsea Man United v Brighton Sheffield au Swansea v Rochdale au Tottenham Wigan au Manchester City v Southampton