Rais FIFA awasili Tanzania

Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) Gianni Infantino amewasilia jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo kwa ajili ya mkutano utakaofanyika leo.

Infantino amefuatana na Rais wa shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) Ahmad Ahmad.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe aliongoza mapokezi kwenye Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Kabla ya kuja Tanzania, Rais wa FIFA alikwenda kwenye nchi za Nigeria na Ghana.