Sijawahi kuumia kuachwa- Wolper

NYOTA wa filamu nchini, Jacqueline Wolper amefunguka kuwa licha ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume tofauti na kubwagana nao, kamwe hajawahi kuumia.

Wolper aliwahi kutoka kimapenzi na msanii wa lebo ya wasafi, Harmonize kabla ya kubwagana hivi karibuni na kila mtu kufanya mambo yake.

Mwigizaji huyo amekuwa na kawaida ya kuwaanika wanaume aliokuwa akiingia nao kwenye uhusiano ili watu wote wajue akidhani itakuwa ngumu kusalitiwa lakini ikawa kinyume chake na kuachana nao.

Alisema, jambo hilo hajawahi kujutia au kuumia kwa kuwa akiachana na mtu anaangalia waliopo kwenye foleni anachagua tu anayemtaka.

"Siwezi kuumizwa na kuachana kwa kuwa unakuta wengi wako kwenye foleni naangalia mwenye sifa za kuwa nami sichagui ana kazi au fedha naangalia mwenye mapenzi,” alisema Wolper.

Hata hivyo alisema kwa sasa hataki tena mahusiano na watu maarafu na anajuta kuwa na watu ambao tayari aliwatangaza na kusema kwa sasa hawezi tena kufanya hivyo.