Simba yaipiku Yanga mapato

KLABU ya Simba imeipiku Yanga katika mapato ya mlangoni kwenye mechi za kimataifa zilizochezwa mapema wiki hii.

Yanga ilicheza na Township Rollers ya Botswana Jumanne wiki hii Machi 6 ikiwa ni mchezo wa Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika na kunyukwa mabao 2-1 wakati Simba ilicheza Kombe la Shirikisho na Al Masry Jumatano Machi 7, na kutoka sare ya mabao 2-2. Mechi hizo zimefanyika kwenye Uwanja wa Taifa, ambapo mchezo wa Simba uliingiza mashabiki wengi zaidi ya Yanga baada ya kuingiza kitita cha Sh milioni 85 baada ya mashabiki 14, 798 kudhuria mchezo huo.

VIP A waliingia Watazamaji 250 kwa kiingilio cha Shilingi 20,000 na kupatikana jumla ya shilingi 5,000,000, VIP B na C waliingia Watazamaji 557 kwa kiingilio cha shilingi 15,000 ikapatikana jumla ya Sh 8,355,000, majukwaa ya rangi ya Machungwa, Bluu na Kijani waliingia Watazamaji 13,644 kwa kiingilio cha shilingi 5,000 imepatikana jumla ya shilingi 68,220,000 Akitoa mchanganuo wa mapato hayo, Ofisa habari wa TFF, Cliford Ndimbo alisema Simba imepata shilingi 43, 585, 346 baada ya kukatwa VAT 12,972,966.10, Selcom 5,017,655.00, TFF 3,352,718.94 na gharama za uwanja 10,058,156.83, gharama za mchezo 6,034,894.10, BMT 670,543.79 na CAF 3,352,718.94 Kwa upande wa Yanga, Ndimbo alisema kuwa timu hiyo ya mtaa wa Jangwani ilihudhuriwa na mashabiki 9,961 na kuingiza Shilingi milioni 56,245,000 na Yanga kuambulia shilingi 28,825,419 baada ya makato mbalimbali na kwamba VIP A wameingia watazamaji 99 kwa kiingilio cha Shilingi 20,000 na kupatikana jumla ya shilingi 1,980,000, VIP B na C waliingia Watazamaji 991 kwa kiingilio cha shilingi 10,000 ikapatikana jumla ya shilingi 9,910,000, majukwa ya rangi ya Machungwa, Bluu na Kijani waliingia Watazamaji 8,871 kwa kiingilio cha shilingi 5,000 imepatikana jumla ya shilingi 44,355,000. Ndimbo akitoa mchanganuo katika mchezo huo alisema VAT 8,579,745.76 Selcom 3,318,455.00, TFF 2,217,339.96, uwanja 6,652,019.89, gharama za mchezo 3,991,211.93, BMT 443,467.99 na CAF 2,217,339.96.