Lipuli yaiduwaza Yanga

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu bara, Yanga jana iliduwazwa na Lipuli kwa kulazimishwa sare ya bao 1-1 katika mechi yake ya kwanza iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Matokeo hayo hayakutarajiwa na wengi kutokana na ugeni wa Lipuli kwenye ligi na hivyo iliingia uwanjani ikiwa haipewi nafasi ya kushinda.

Add a comment