Utafiti wa mboga za majani uimarishwe EAC

T - gonjwa ya virusi kwenye mboga Afrika Mashariki unatia moyo kwa wakazi wa eneo hilo. Hii inatokana na ukweli kwamba familia nyingi zinatumia mboga hizo kwa chakula lakini pia kwa wengine ni zao la biashara linalowaingizia kipato.

Sisi tunaipongeza hatua hiyo yenye kulenga matumizi endelevu ya mbogamboga kwa lengo la kuboresha afya za watumiaji pamoja na kulinda afya zao dhidi ya magonjwa yanayoweza kupatikana kutokana na virusi vya kwenye mboga husika.

Mtafiti wa Tafiti za Virusi vya Mimea anayesimamia mradi wa kupambana na magonjwa ya virusi kwenye mboga Afrika ya Mashariki kwa upande wa Tanzania, Dk Peter Sseruwagi katika mazungumzo na HabariLeo anasema lengo kubwa ni kusaidia wakulima wa mbogamboga nchini kukabiliana vilivyo na virusi hao waharibifu wa mboga.

Hakuna ubishi kwamba wananchi wengi wanatumia mboga za majani katika maakuli mbalimbali kwa siku ikiwa ni pamoja na sukuma wiki, kabichi nyeupe na nyekundu, nyanya, pilipili hoho, nyanya chungu, karoti, spinachi, vitunguu, kunde, biringanya na nyingine nyingi.

Kuna mbolea na aina za dawa mbalimbali zinazotumika kukabiliana na uharibufu lakini pia juu ya usalama wa dawa ambazo wakati mwingine hutumika kudhibti wadudu waharibifu.

Sisi tuna matumaini makubwa na utafiti huo kwa kwamba utotoa ufumbuzi wa kupata mboga safi na zilizo bora kwa matumizi ya binadamu lakini pia kulinda afya za watumiaji dhidi ya dawa zinazotumika kudhibiti uharibifu.

Ni matarajio pia ya wananchi katika kanda hiyo kwamba watafiti husika watakapokamilisha kazi hiyo, watakuwa na nafasi pia ya kutoa mafunzo kwa wakulima wa mboga ili kutumia ipasavyo yaliyogunduliwa katika utafiti wao kuendeleza kilimo endelevu cha mboga.

Tungependa kutoa wito kwa wizara na mamlaka husika katika masuala ya kilimo kuhakikisha kwamba wanawaandaa wataalamu wa kuweza kuwafikishia elimu hiyo wakulima wa mboga ili kuwapatia uwezo wa kujiletea tija katika kilimo hicho.

Hapa kwa upande wa Tanzania, tunazungumzia umuhimu wa kuwaandaa vyema mabwana shamba na mabibi shamba ili kuwa tayari kwa ajili ya elimu kwa wakulima wa mboga ambao wana umuhimu wake katika lishe ndani ya jamii zetu.