Yanga, Simba sasa fikirieni kimataifa zaidi

TIMU za Yanga na Simba zinatarajia kuwakilisha taifa katika mashindano ya soka ya kimataifa, ambayo huendeshwa na Shirikisho la Soka la Afrika (Caf).

Yanga itashiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika wakati watani zao Simba, wenyewe watacheza Kombe la Shirikisho la Afrika. Kwa miaka mingi timu hizo pamoja na Azam FC katika miaka ya hivi karibuni, zimekuwa ndio wawakilishi wakubwa wa Tanzania katika mashindano hayo.

Kwa msimu huu, Yanga na Simba ndio watashiriki mashindano hayo, na tayari ratiba ya awali imeshatoka. Klabu hizo kongwe nchini ukiondoa Azam FC, ambayo haina hata miaka 20 tangu ianzishwe, zimekuwa zikifanya vibaya mara kwa mara katika mashindano ya kimataifa, lakini zimeshindwa kujifunza kutokana na makosa.

Tofauti na ukongwe wake, timu hizo, zimeshindwa kabisa kupata mafanikio kimataifa ukilinganisha na klabu za nchi nyingine kama Congo, Misri, Tunisia, Nigeria, Cameroon, Ivory Coast na kwingineko.

Maandalizi ya timu hizo kongwe bado siyo ya kushiriki na kufanya vizuri katika mashindano hayo ya kimataifa ila ni kwa ajili ya kushiriki na kusindikiza tu na ndiyo maana zinatolewa mapema kabisa zinapofi ka mzunguko wa kwanza na kupangwa na timu kutoka baadhi ya nchi tulizozitaja awali.

Tunakumbuka wakati Simba inacheza hadi kufi kia fainali ya Kombe la Caf wakati ule mwaka 1993, timu hiyo ilipiga kambi nje ya nchi mara nyingi na iliwasaidia kuzifunga timu kubwa barani Afrika.

Hata Yanga miaka ya nyuma iliwahi kufanya vizuri barani Afrika, lakini miaka ya hivi karibuni nayo imekuwa yale yale. Timu hizo zote zina zaidi ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwake, lakini kimaendeleo ziko nyuma kama vile vilianzishwa miaka miwili au mitatu iliyopita.

Pamoja na kufanya vibaya kwa miaka mingi katika mashindano ya kimataifa, timu hizo mbili hazioneshi jitihada za kutaka kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa msimu huu. Katika timu hizo, kikubwa kinachoonekana ni kujiandaa zaidi kwa mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara ili kutwaa taji au kumfunga mtani wake pale watakapokutana katika ligi hiyo na siyo kimataifa.

Tatizo la Simba na Yanga ni ile tabia yao ya kutaka kuwa mwamba wa mwenzake tu na siyo kutamba kimataifa na hali hiyo imejengeka hata kwa mashabiki wao, wachezaji na wengine wanaozishabikia timu hizo.

Ili uwe kiongozi mzuri au mchezaji mzuri wa moja ya timu hizo, wewe wafunge tu watani zenu, basi hapo maisha utakuwa umeyapatia na hakuna wakukusumbua. Wakati umefi ka kwa Simba na Yanga kuacha kufi kiri kufanya vizuri katika Ligi Kuu Tanzania Bara pekee, badala yake wafi kirie pia mashindano ya kimataifa