Karibu sana Rais wa Misri

Rais wa Misri, Abdel Fattah Al Sisi aliwasili nchini jana kwa ziara ya siku mbili. Ziara yake hiyo, inafuatia mwaliko wa Rais John Magufuli wakati wa mazungumzo yao mwanzoni mwa mwezi Januari mwaka huu wakati walipokutana jijini Addis Ababa nchini Ethiopia, wakihudhuria kikao cha 28 cha wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU).

Add a comment