Infantino agomea kadi ya bluu

FIFA inapinga pendekezo la Bodi ya Shirikisho la Soka la Kimataifa la kuazishwa kwa ‘kadi ya bluu’, Rais Gianni Infantino amesema.

Pendekezo la bodi ya sheria ya mpira wa miguu kuanzishwa kwa kadi ya bluu ambayo inawapa waamuzi uwezo wa kuwatoa wachezaji kwa dakika 10 kwa kufanya makosa ya kejeli, ilijadiliwa na FIFA katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa IFAB huko Scotland.

“Hakutakuwa na kadi zozote za bluu. Hii ni mada ambayo haipo kwetu,” Infantino aliwaambia waandishi wa habari jana jioni, alipowasili kwenye mkutano wa IFAB huko Loch Lomond Scotland.

“FIFA inapingana kabisa na kadi za bluu. Sikujua mada hii kama rais wa FIFA. Nadhani FIFA ina usemi katika IFAB.”
Infantino amesema siku zote FIFA itakuwa mbele kuangalia mawazo na mapendekezo, lakini wakati mwingine ni bora kulinda kiini na jadi ya mchezo wa mpira wa miguu.

Habari Zifananazo

Back to top button