Infantino akutana na Vini Jr, atoa maagizo ubaguzi

“Hatuwezi kuvumilia” hatua lazima zichukuliwe dhidi ya vitendo vya ubaguzi kwenye soka, na waamuzi wote lazima wasimamishe mchezo vitendo hivyo vinapotokea,” Rais wa FIFA, Gianni Infantimo amesema.

Infantino amesema hayo leo alipokutana na mshambuliaji wa Real Madrid, Vinícius De Oliveira ‘Vini Jr’ kujadili masuala ya ubaguzi huku Vini akieleza namna alivyozukutana na mkasa wa ubaguzi wa rangi mwenye uliopita katika mchezo dhidi ya Valencia.

Mkuu huyo wa FIFA aliwaita wabaguzi kuwa ni ‘jinai’ na kuzitaka mamlaka za soka ulimwenguni kote kuchukua hatua dhidi yao.

Vinicius, ambaye ni mweusi, amekuwa akilengwa na ubaguzi wa rangi na mashabiki katika viwanja vya Uhispania kwa msimu mzima, bila ya waamuzi au mashirika ya soka kumlinda.

 

Mwezi uliopita, Real Madrid iliwasilisha malalamishi kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Uhispania ikidai unyanyasaji wa kibaguzi wa Vinicius ni uhalifu wa chuki baada ya mchezaji huyo kukumbana na sakata hilo dhidi ya Valencia.

Habari Zifananazo

Back to top button