Infantino awasili Burundi
Rais wa FIFA, Gianni Infantino amewasili Bujumbura, Burundi kwa ya ziara yake ya kikazi.
Infantino ameongozana na Mosengo Véron ambaye ni Katibu Mkuu wa CAF, Pierluigi Collina (Rais wa Kamati ya Waamuzi) pamoja na Arsène Wenger ambaye ni Mkuu wa Maendeleo ya Soka Duniani.
Kiongozi huyo amewasili nchini humo akitokea Tanzania ambako alishuhudia mchezo wa African Fototball League kati ya Simba na Al-Ahly ulioisha kwa sare ya mabap0 2-2 uwanja wa Mkapa jana.