Infantino huyu hapa Tanzania

RAIS wa FIFA Gianni Infantino amewasili nchini leo asubuhi kwa ajili ya ufunguzi wa mchezo wa African Football League kati ya Simba Sc dhidi ya Al Ahly ya Misri utakaochezwa Mkapa Saa 12:00 Jioni.



Infantino amewasili na kupokewa na Makamu wa Kwanza wa Rais TFF, Athuman Nyamlani.



Katibu Mkuu wa FIFA, Fatma Samoura atakuwa miongoni mwa wageni watakaoshuhudia mchezo huo.

Advertisement


Rais wa Shirikisho la Soka Amerika Kusini, Alejandro Dominguez pia atakuwepo. Kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger pia atahudhuria mchezo huo.

1 comments

Comments are closed.